Home » » WATAALAMU WA AFYA VIJIJINI WAPEWA VITENDEA KAZI.

WATAALAMU WA AFYA VIJIJINI WAPEWA VITENDEA KAZI.


Julai 23, 2024

Zaidi ya  watoa huduma za Afya  Tisa  kwenye vijiji vilivyo mbali kwa Kilomita 5 kutoka eneo la kituo cha kutolea huduma za Afya wamepewa vitendea kazi ambavyo vitawasaidia  kurahisisha utekelezaji wa Majukumu yao.

Akigawa vifaa hivyo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Francis Mkuti amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za Afya na kuhakikisha kila Mwananchi anapata huduma hiyo popote alipo.

Aidha, Mkuti amewasisitiza wataalamu hao kuvitumia vyema vifaa hivyo ili vilete tija katika kuwahudumia Wananchi.

Awali akitoa taarifa ya Vitendea kazi  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Dkt. Adorat Mpollo amevitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na  Baiskeli , Mizani , Kipimajoto ,Stop watch ,Simu Janja  na Vishikwambi ambavyo vyote vitawasaidia iwapo Kuna mgonjwa Yuko eneo la Kijiji waweze kumfikia haraka na kumpatia huduma ya Afya.

#kaziiendelee

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa