Julai 29, 2024
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Francis Mkuti ameongoza Kikao Cha Robo ya Nne Cha kijadili Utekelezaji wa Viashiria vya Mkataba wa Lishe na kuwapongeza Viongozi hasa Watendaji wa Kata kwa kusimamia vyema na kuhakikisha Jamii inakuwa na lishe Bora na kuimarisha Afya zao.
Awali akitoa taarifa ya robo ya Nne(Aprili-Juni 2023/ 2024) Afisa Lishe Wilaya ya Tandahimba Asha Selemani amesema Shule za Sekondari na Msingi zote Wilaya ya Tandahimba zinapata Chakula walau Mlo mmoja kwa siku , na wamefanikiwa kudhibiti utapiamlo kwa 100% kwa watoto wenye Umri Chini ya miaka mitano sambamba na kufanikiwa kuelimisha jamii ulaji Bora wa Mlo kamili.
Aidha, Mkuti amewasisitiza watendaji wa Kata kuendelea na kasi hiyo na zaidi kwa kutoa Elimu kwa Jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe Bora .
Katika Robo ya Nne Kata ya Mihambwe imeongoza kwa 95.54% utekelezaji wa Mkataba wa afua za Lishe kati ya Kata 32 za Wilaya ya Tandahimba.
#kaziiendeleeš„

0 comments:
Post a Comment