Home » » ZIARA YA MBUNGE KATANI YAACHA TABASAMU MKOREHA.

ZIARA YA MBUNGE KATANI YAACHA TABASAMU MKOREHA.



Tandahimba -Mtwara

Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani A. Katani amesema Serikali imejipanga vyema kutoa pembejeo za kilimo cha zao la Korosho kwa Wananchi kulingana na Ukubwa wa Shamba  na idadi ya Mikorosho aliyo nayo Mkulima .

Mhe.Katani ametoa kauli hiyo kwenye Mkutano wa hadhara wakati akisikiliza na kutatua kero za Wananchi  katika Kata ya Mkoreha  baada ya Wananchi kuwa na hofu juu ya Ugawaji wa Pembejeo ambayo haikidhi mahitaji ya Wakulima .
"Niwahakikishie Wananchi kwamba tutahakikisha Wakulima walioandikisha Ukubwa wa Shamba na  Idadi ya Miti ya Korosho  wanapata Mifuko ya kupuliza  inayoendana na Ukubwa wa Shamba" Mhe.Katani

Katika Suala la Umeme Mhe.Katani amesema tayari miundombinu ya Umeme imewekwa na hivi karibuni Wananchi watapata huduma ya umeme katika Vijiji vya Kata hiyo.

Akijibu Swali la Mwananchi  kuhusu  kukamilika kwa Zahanati ya Chikongo,  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Dkt. Adolati Mpolo amesema Serikali imetoa fedha kiasi Cha Tsh.Milioni 50 Kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya miundombinu ili Wananchi wapate huduma za Afya karibu na maeneo yao.

Mhe.Katani akiambatana na Wataalamu anaendelea na ziara ya Siku 15 katika Kata za Wilaya ya Tandahimba akisikiliza, kutatua na kufafanua  kero za Wananchi wa Jimbo la Tandahimba.

 


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa