Ikiwa
ni mkutano wa mwisho wa Baraza la Madiwani kwa mwaka wa fedha 2023/2024
kupokea na kujadili taarifa za Maendeleo za kata kwa robo ya nne, Leo
tarehe 30/07/2024 Kata ya Dinyecha imewasilisha ombi la vijiji viwili
Chikwaya na Kibaoni kupewa hadhi ya mitaa. Kwa sasa kata ya Dinyecha Ina
Vijiji viwili, Mitaa mitatu na Vitongoji 11.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba, Eng. Mshamu A. Munde aliahidi kutuma timu ya wataalamu kuangalia ikiwa vijiji hivyo vina sifa ya kuwa mitaa kabla ya kupeleka ombi hilo ngazi za juu kwaajili ya mchakato zaidi.
Akitoa maoni kuhusu taarifa za maendeleo za kata zilizowasilishwa Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Mhe. Abdallah Dadi Chikota aliwataka wajumbe kuonesha miradi ya maendeleo zinazotekelezwa katika kata zao bila kujali chanzo cha fedha au taasisi wezeshi.
“Mfano kata ya Kitaya kuna mradi mkubwa wa maji utakaotoa maji kijiji cha Maembejuu kwenda Mchanje mpaka kijiji cha Maembechini ambao tayari umefikia 80% lakini kwenye taarifa haijaoneshwa. Hata kule kata ya Nyundo kuna ujenzi wa Zahanati na kijiji cha Niyumba pamoja na ujenzi wa shule fedha za BOOST taarifa haijaainisha hayo.”Alisema Mhe. Chikota
Katika hatua nyingine Mkurugenzi amewataka watendaji wa kata kuhakikisha makusanyo katika kata zako hayashuki 80% kwa ustawi mzuri wa Halmashauri.

0 comments:
Post a Comment