Home » » KILIMO BORA CHA KOROSHO

KILIMO BORA CHA KOROSHO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


UTANGULIZI
koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae karne ya 16 ndipo ilipo fika africa katika nchi ya mozamboque na baadae ikafika Kenya na Tanzania.

kwa hapa Tanzania kilimo cha korosho hulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya kusini ukiwepo mkoa wa Mtwara.

Je ni mvua kiasi gani na udongo gani unafaa kulimwa zao hili?

mvua inayotakiwa wakati wa kulima zao la korosho: korosho ustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua zinazo tiririka kwa milimita 840mm hadi 1250mm ambazo ni mvua za wastani kwa mwaka.

Pia zao hili hukua vizuri maeneo yenye ukanda wa 0- 500m kutoka usawa wa bahari.

udongo wa aina gani; korosho hukua vizuri kwenye maeneo yenye udongo wa PH 5.6 ambao ni udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi.
NAMNA YA KUANDAA SHAMBA 
Shamba la korosho linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajiri ya kupanda korosho,pia katika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya mboji ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.
KUPANDA
 Ni muhimu sana   kuchagua mbegu bora kwa kua mbegu utakayo panda ndo itakuonesha kiasi gani utavuna,
  • baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g unaweka katika maji yenye kiasi cha lita 5 unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kuota,
 baada ya hapo unazianika vizuri ili ziweze kukauka
na pia unashauriwa kuto panda mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja,
nafasi ya kupanda 12m x 6m kwenye maeneo yenye mvua kiasi na miti hekali moja kitakua 139/
kwenye maeneo yasio na mvua za kutosha ni 12m x 12m na kiasi cha miti ni 69 kwa hekali moja

MUHIMU
Kuna aina mbili ya kupanda mbegu ya korosho
  • kupanda moja kwa moja; hii ni njia mambayo ni risk sana na inahitaji umakini kwa sababu  kunauwezekano mkubwa wa mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu 3 katika shimo moja na baada ya miezi mi 3 - 4 ng'oa mimea na bakiza mmoja wenye afya na muonekano mzuri.
  • njia ya kitaru; hii ni njia ya pili na ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na muonnekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye afya.
na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuathiriwa na magonjwa au wadudu na yale yalio kauka.

KUVUNA
Korosho ifikia hatua ya kuzaa matunda pale inapo kua na umri wa mwaka  2 hadi miaka mitatu
napia matunda hukomaa pale inapo kua na miaka 9 hadi 10
uwezekano wa mkoroso kuishi ni miaka 30 hadi 40
na kuvuna hua kunaanza mwezi wa october hadi mwezi december 

MATUMIZI YA KOROSHO
  • chakula 
  • hutumika kutengeneza rangi
  • kama zao la biashara
  • miti yake hutumkia kama kuni NK

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa