Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi
(kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi
wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Matumizi
Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang'a , Meneja Ofisi Kuu ya
Utabiri, Samwel Mbuya, pamoja na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk.
Hamza Kabelwa.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania leo imewapa semina baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema semina hiyo ni utaratibu wa TMA kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwa mabalozi wa zuri wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi.

Alisema
wanahabari inabidi wazielewe vizuri, kuzichambua na kuwafikishia
taarifa za utabiri wa hali ya hewa kiusahihi wananchi jambo ambalo
litasaidia wananchi na sekta mbalimbali kujipanga kukabiliana na ama
athari zitokanazo na utabiri wa hali ya hewa.
"...Semina
kama hizi kwanza zinasaidia wanahabari kuelewa masuala mbalimbali
yatokanayo na taarifa zetu za utabiri, kisha wao kuelimisha jamii zaidi
kuhusiana na taarifa zetu kupitia vyombo vyao mbalimbali vya habari.
Kundi hili likielewa vizuri nao watakuwa mabalozi wazuri kufikisha
ujumbe kupitia kalamu zao," alisema Dk Agnes Kijazi.
Aidha
pamoja na mafunzo hayo, TMA pia ilipokea mrejesho na ushauri kutoka kwa
wanahabari ili kuboresha zaidi namna ya utoaji wa taarifa za utabiri wa
hali ya hewa kwa umma.
Picha ya pamoja ya washiriki wa semina kwa baadhi ya waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za
hali ya hewa.
0 comments:
Post a Comment