TBA YATAKIWA KUHAKIKISHA MAENEO YAO YANA HATI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala huo, mkoani humo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), mkoa wa Mtwara Edward Mwangasa, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, katika ukaguzi wa nyumba zinazomilikwa na Wakala huo ambao unamiliki jumla ya nyumba 76 mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, wakati alipokuwa akikagua nyumba zinazomilikiwa na Wakala wa Majengo (TBA), mkoani humo.

……………………

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ametoa agizo kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha wanazitambua na kuzisajili nyumba zote na viwanja vya Serikali zinazomilikiwa na Wakala huo katika maeneo mbalimbali nchini.

Agizo hilo amelitoa mkoani Mtwara, mara baada ya kukagua nyumba na viwanja vinavyomilikiwa na Wakala huo na kusisitiza kwa Mameneja wa mikoa wa Wakala huo kuhakikisha wanafanya matengenezo na ukarabati wa majengo hayo ili kuvutia wapangaji wao.

“Wasimamizi wa nyumba hizi hakikisheni nyumba hizi mnazitambua na mnazifanyia matengenezo ya mara kwa mara, nimetembelea Halmashauri mbalimbali na kuona baadhi ya nyumba za Serikali haziridhishi baada ya kuwa zimetelekezwa muda mrefu”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo amemtaka Kaimu Meneja wa TBA mkoani Mtwara, kuhakikisha nyumba na viwanja vyote anavyosimamia vinakuwa na hati ili kidhibiti changamoto ya wananchi kuvamia viwanja vya Serikali.

Amekemea tabia ya baadhi ya wapangaji wa nyumba za Serikali kutozitunza wala kuzijali nyumba hizo hali inayoipelekea Serikali kuingia gharama kubwa katika kufanya marekebisho ya nyumba hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TBA mkoani hapo, Edward Mwangasa, amekiri kutokuwa na hati kwa baadhi ya nyumba na viwanja wanavyovimiliki na hivyo amemuahidi Naibu Waziri huyo kuhakikisha anasimamia suala la utafutaji wa hati kwa nyumba hizo na viwanja vyote 128 walivyonavyo sasa.

“Mheshimiwa Naibu Waziri nakuhakikishia kulifanyia kazi suala la ufuatiliaji wa hati za nyumba na viwanja ili kuweza kuepuka migogoro na wananchi wanaovamia viwanja vyetu”, amesitiza Kaimu Meneja.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amewataka wananchi kufuata sheria na kwamba hairuhusiwi kuvamia maeneo ya Serikali kwani maeneo hayo huwa yanatengwa kwa ajili ya shughuli za Serikali.

Wakala wa Majengo Mkoani Mtwara una jumla ya nyumba 76 ambapo Manispaa ya mji wa Mtwara ina nyumba 64, Masasi 4, Nanyumbu 5 na Tandahimba 3 ambapo baadhi ya nyumba hizo zina hati na nyingine hazina.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

NAPE AFUNGUKA AKIMNADI DK. NDUMBARO ADAI KAMWE HATA IHAMA CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Nape akibadilishana mawazo na Dk. Ndumbaro
Na Gideon Mwakanosya-Songea


MBUNGE wa jimbo la Mtama mkoa wa Lindi Nape Nnauye amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kukihama chama cha mapinduzi (CCM) kama baadhi ya watu wakiwemo wa vyama vya upinzani  kwa kile alichodai kuwa  magari ya upinzani yanaenda kuzama na hayajulikani yataibuka lini.
Uwazi huo ameuweka jana wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma kwa tiketi ya CCM Dk, Damas Ndumbaro kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya bombambili Manispaa ya Songea.
Nnauye ambaye aliwahi kuwa katibu wa hitikadi na uenezi CCM taifa na Waziri wa Habari, Michezo na Sanaa katika serikali ya awamu ya tano alisema kuwa kama kuna watu walidhani atakihama chama cha mapinduzi (CCM) na kwenda upinzani wasahau kabisa .
Akizungumza kwa kujiamini huku akishangiliwa na mamia ya wakazi wa bombambili alisema kuwa kama kuna kuwa na matatizo ndani ya CCM tunaonyana ndani ya chama na kuyamaliza na siyo kuhama chama.
“Naikubali serikali ya awamu ya tano inayongonzwa na jemedali Dk. John Magufuli pamoja na makamu wa Rais na waziri mkuu wake kuwa ipo imara na mimi naapa kufia CCM na siyo vinginevyo” alisema Nape Nnauye.
“Nasikia maneno maneno kutoka kwa baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na mawazo hayo” alisema mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
Katika kampeni hizo ambazo uchaguzi wake utafanyika Januari 13 mwaka huu Nape Nnauye na Moses Machali aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Kasulu mkoa wa Kigoma kwa tiketi ya NCCR Mageuzi wamekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa jimbo la Songea hasa wanapokuwa majukwani.
  MWISHO.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO MHE MWANJELWA AMPA MRAJISI SIKU 7 ZA KWANINI MAGUNIA KUTOFIKA KWA WAKATI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017. Picha na Mathias Canal
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa akimuonyesha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa jinsi magunia yalivyopangwa kwa ustadi ktika gala la kuhifadhia Korosho la Mtanda mara baada ya  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017.
Badhi ya wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) wakifatilia mnada wa tano wa korosho katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara. Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakiwasili Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kwa ajili ya kujionea Mnada wa Korosho unavyoendeshwa, Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa Tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wazee maarufu wa kijiji cha Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa (Wa Kwanza Kushoto), na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia (Wa Kwanza Kulia).
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakati wa Mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia wakati wa ukaguzi wa ghala la Buko Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara  wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Humo, Jana Novemba 17, 2017
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza ushauri sambamba na pongezi kwa kushiriki Mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara  wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Humo, Jana Novemba 17, 2017
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakikagua magunia ambayo tayari yamewasili katika Ofisi ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama Kikuu cha ushirika mara baada ya kumalizika kwa mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.

Na Mathias Canal, Mtwara

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa leo Novemba 18, 2017 amemuagiza Mrajisi wa vyama vya ushirika kukamilisha haraka kazi ya uchunguzi kwenye Bodi za vyama vya ushirika vya Mkoa wa Mtwara ili kubaini sababu zilizopelekea kuuzwa kwa magunia kiholela.

Alisema kuwa kumalizika kwa uchunguzi huo kutarahisisha kuchukuliwa haraka hatua kali za kisheri kwa wale wote watakaobainika kukiuka sheria No 17 ya vyama vya ushirika.

Naibu waziri alitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kugundua kuwa kuna viashiria vya ukiukwaji wa taratibu katika upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia korosho wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.

Sambamba na hilo Naibu waziri Mhe Mwanjelwa wakati wote wa mkutano huo ameshuhudia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) kuhusu ucheleweshwaji wa upatikanaji wa maguni kutoka kwa mzabui, Mapungufu ya kilo kati ya PDA na WHRs ghala kuu, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa malipo ya wakulima kwa njia ya benki kutoka kwa wanunuzi.

Katika ziara yake hiyo kilio cha wananchi wengi na wakulima walisiitiza zaidi kuhusu kukosekana kwa magunia hayo huku wakieleza kuwa wakati mwingine kuchelea kufika ama kutowafikia kabisa jambo ambalo linachangia kupunguza thamani ya zao la korosho.

“Nataka Mrajisi ufanye na ukamilishe kazi yako ya uchunguzi na baada ya kuipata taarifa hiyo hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wote watakaogundulika kukiuka sheria ya nchi” Amekaririwa Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa

Mbali na agizo hilo Naibu Waziri pamoja na wabunge wa Mkoa wa Mtwara walipata nafasi ya kujionea mnada wa tano wa ununuzi wa korosho unavyoendelea.

Hata hivyo Mnada wa tano ulishuhudiwa Kilogramu 7,524,104 za korosho zikiuzwa kwa thamani ya zaidi ya Bilioni 30.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa amesema Wizara itayafanyia kazi haraka mapendekezo ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa kufanya uchunguzi kuhusu mwenendo mzima wa magunia pamoja na upatikanaji wake.

KUBEZA DHANA YA VIWANDA NI MTAZAMO FINYU NA ULIOPITWA NA WAKATI-WAZIRI JENISTA MHAGAMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKURUGENZI WA ILEJE ATEMBELEA KILWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai kulia akisalimiana na mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Haji Mnasi ,mara baada ya Mkurugenzi huyo kufika ofisini kwake jana kwaajili ya kumsalimu  kushoto ni Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Zabron Bugingo(Picha na Pamela Mollel Kilwa)


Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai kulia akisalimiana na mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Zablon Bugingo katikatimkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe  

NAIBU WAZIRI KAKUNDA AFANYA ZIARA KILWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo kulia akitoamaelezo ya mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai 
Afisa kilimo na ushirika wilaya ya Kilwa John Mkinga kushoto akitoa taarifa ya mradi wa uoteshaji wa miche ya korosho mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo
Picha ikionyesha viriba vya kuoteshea miche ya korosho
Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda akiingia katika eneo la uoteshaji wa miche ya korosho,kushoto ni Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai 


Pamela Mollel,Kilwa

Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda amewataka viongozi wa serikali wilayani Kilwa Mkoani Lindi kuhakikisha wanasimamia vyema upandaji wa miche mipya yazao la korosho hali ambayo itaongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wananchi na kuinua uchumi wa Taifa

Hayo aliyasema jana wilayani Kilwa wakati wa ziara yake baada ya kuelezwa kuwa mkakati wa wilaya uliopo ni kuhakikisha wanazalisha na kupanda miche milioni moja kila mwaka hali ambayo itaongeza mashina ya zao hilo kutoka laki sita yaliyopo na zaidi kutokana na mpango huo kuwa wakudumu

Kufuatia hali hiyo Kakunda alisema ili miche hiyo iote vizuri na kustawi lazima uwepo usimamizi mkubwa kwa viongozi wote wa serikali wilayani humo kuliko kuacha usimamizi kwa wakulima peke yao ambao wanaweza kusababisha kukauka na kushindwa kufikia malengo

Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo alisema tayari hatua za awali za kuotesha miche milioni moja kila mwaka zinaendelea ambazo miche hizo itagawiwa bure kwa wakulima hali ambayo itainua uchumi wao

Bugingo alisema mpango huo ni wakudumu ambapo kila mwaka wilaya itazalisha miche hiyo milioni moja na kuigawa kwa wakulima bure hali ambayo itakuwa zaidi ya mara mbili ya uzalishaji wa miche iliyopo ambayo kwa sasa ni laki sita tu iliyowaingizia shilingi Bilioni 13 na halmashauri kujipatia zaidi ya shilingi milioni220

Aliongeza kuwa mbali na kujipatia fedha kwa wakulima pia halmashauri itajiongezea mapato ya ushuru baada ya serikali kufuta baadhai ya vyanzo ikiwemo ya mabango iliyorudishwa serikali kuu hivyo zao hilo la korosho linaweza kuingizia halmashauri zaidi ya shilingi bilioni 40 kutokana na mpango huo kuwa zaidi ya mara mbili zaidi

Mbali na hali hiyo Waziri Kakunda ameupongeza mpango huo wa upandaji wa miche hiyo milioni moja kila mwaka kutokana na kuvuka malengo ya serikali ya kupanda miche elfu 50 kwa kila wilaya inayolima zao la korosho ingawa Afisa kilimo na ushirika wa halmashauri hiyo ya Kilwa John 

Mkinga amesema changamoto iliyopo ni ucheleweshwaji wa mbegu hali inayosababisha zoezi la uoteshaji miche hiyo kwenda taratibu ingawa Kakunda amesema atawasiliana na wizara ya kilimo kumaliza tatizo hilo

IGP SIRRO AWAKUMBUSHA ASKARI WAJIBU WAO WA KUTENDA HAKI WANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na maafisa wa Polisi alipowasili katika mkoa wa Mtwara, leo kwa ziara ya siku moja ya kikazi yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akimsikiliza Kmamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya, leo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari nje ya Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Mtwara, akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi alipowasili mkoa wa Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoa wa Mtwara, mara baada ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake. IGP Sirro, yupo mkani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la kuzumgumza na askari pamoja na kuwakumbusha wajibu wao wa kutenda haki wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi za Polisi. Picha na Jeshi la Polisi.

DKT. HARRISON MWAKYEMBE AZINDUA MPANGO WA USAJILI NA UTOAJI VYETI KWA WATOTO WALIOCHINI YA UMRI MIAKA MITANO KWA MIKOA YA MTWARA NA LINDI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 25,2017

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa