Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Tandahimba Mshamu Bakiri amezindua Mradi wa Chumba Cha Kompyuta Shule ya Sekondari Luagala Kwa ajili ya wanafunzi wa Shule hiyo kuweza kujifunza Masomo yao pamoja na kuwa na Ujuzi wa TEHAMA.
Mradi wenye Gharama ya Tsh.Milioni 70 ukijumuisha Chumba Cha kompyuta, Meza na Kompyuta 25 umefadhiliwa na Taasisi ya CAMARA EDUCATION TANZANIA ambayo imelenga kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji, kuongeza Ujuzi wa matumizi ya Kompyuta na TEHAMA na hatimaye kuzalisha wataalamu wenye Ujuzi wa TEHAMA hapo baadae.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Francis Mkuti amewaasa Wanafunzi akisema
" Mkiitumia Vizuri ufaulu utaongezeka na tunawadai matokeo,hatutarajii kupata Sifuri kwa kuwa Mazingira yameboreshwa"
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo DCI.Mariam Mwanzalima amewashukuru wafadhili hao kuwa sehemu ya kuboresha Miundombinu ya Sekta ya Elimu akisisitiza Wanafunzi kutumia Kompyuta hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Katika Uzinduzi huo Viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, baadhi ya Madiwani na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Elimu .
#kaziiendelee

0 comments:
Post a Comment