Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mtaalam
kutoka Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
ya GASCO inayojihusisha na usambazaji wa gesi, Mhandisi Mwanaidi Rashid
(kulia) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo Namba I cha gesi
ambapo Kiwanda cha Saruji cha Dangote kitaunganishwa na huduma hiyo kwa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo ( wa tatu kutoka kulia mbele) na Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia ( wa nne kutoka kulia mbele)
wakiwa katika picha ya pamoja na kamati hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha
(kulia) akimpokea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) aliyeambatana na Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Bajeti mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha
(kulia) akielezea mafanikio na changamoto za kiwanda hicho kwa wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti (hawapo pichani). Wengine kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa
Ghasia na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo, akifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa
Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (hayupo
pichani ) katika kikao hicho.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha
(mbele) akielezea jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika
kikao kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda hicho.
Sehemu
ya wajumbe kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na watendaji wa
kiwanda cha Dangote wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra
Raithatha (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Kutoka
kulia mbele mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Mhandisi Edson Ngabo,
Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango, Josephat Mbwambo na Kaimu
Mkurugenzi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
wakifuatilia maelekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge katika kikao hicho.
Mchumi
kutoka Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Josephat Mbwambo (kulia) akinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa
zinawasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika
kikao hicho.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja akifafanua jambo katika
kikao hicho
0 comments:
Post a Comment