Home » » SHIRIKA LA SPORTS DEVELOPMENT AID (SDA) YAGAWA VIFAA VYA MICHEZO MJI NANYAMBA.

SHIRIKA LA SPORTS DEVELOPMENT AID (SDA) YAGAWA VIFAA VYA MICHEZO MJI NANYAMBA.



SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sports Development Aid (SDA) leo tarehe 9/7/2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nanyamba.

Sports Development Aid wamegawa vifaa hivyo vya michezo kupitia  mradi wa Empowered Girls Speak Out (EGSO).

Akizungumza mbele ya mgeni Rasmi mratibu wa mradi huo kwa Mji Nanyamba Bi Amina Banda alisema kuwa shule sita za Mji Nanyamba ambazo zinanufaika na mradi huo ni Nanyamba Sekondari, Mnima Sekondari, Mtimbwilimbwi Sekondari, Mbembaleo Sekondari, Kiromba Sekondari, Mnyawi Sekondari pamoja na shule Moja ya watoto wenye mahitaji maalum ambayo shule ya Msingi Dinyecha.

Mgeni Rasmi katika zoezi hilo la ugawaji vifaa hivyo alikuwa  Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa kata ya Kitaya Mhe Jamali Kapende alilishukuru shirika hilo la SDA na kuwaeleza wanufaika wamepewa vifaa hivyo waende wakavitendee haki kwa kuibua vipaji kwenye shule zao alimalizia kwa kusema maneno hayo hayo.

Vifaa vilivyotolewa na shirika hilo ni mipira ya miguu mitatu kwa Kila shule, mipira mitatu ya Mpira wa mikono kwa Kila shule, mipira mitatu ya Handball kwa Kila shule, Filimbi, koni, tufe, Kisahani kwa shule zote.

 


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa