Home » » MJI NANYAMBA YAMWAGA ZAWADI KWENYE MAADHIMISHO LA JUMA LA ELIMU KIHALMASHAURI.

MJI NANYAMBA YAMWAGA ZAWADI KWENYE MAADHIMISHO LA JUMA LA ELIMU KIHALMASHAURI.



Katika kuelekea kwenye kikele Cha juma la Elimu Halmashauri ya Mji Nanyamba Jana tarehe 9/7/2024 imeadhimisha maadhimisho hayo Kihalmashauri katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nanyamba.

Maadhimisho hayo ya juma la Elimu Kihalmashauri mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Mhe Jamali Abdalla Kapende na kutoa zawadi kwa shule Bora zilizofanya vizuri matokeo katika mtihani wa Taifa kwa shule za Msingi na Sekondari mwaka 2023/2024 kwa kushika nafasi ya pili kwa Mkoa wa Mtwara.

Zaidi ya millioni 10.7 Halmashauri wametoa kwa shule Bora sita, tatu za Msingi na tatu za Sekondari, wanafunzi watatu waliofanya Vizuri na kutoa Madawati kwa shule kumi za Msingi kupitia mfuko wa elimu.

Afisa Elimu Sekondari Ndg Seif A. Mokiwa alizitaja shule hizo ni Njengwa Sekondari, Nanyamba Sekondari na Mbembaleo Sekondari kwa Upande wa Sekondari na shule za Msingi ni Mnyahi, Mbambakofi na Nanyamba Ufundi. Kwa shule zilizopewa madawati kwa lengo la kupunguza uhaba huo alizitaja shule hizo za Msingi ambazo ni Malamba, Namkuku, Azimio, Hinju, Mnima, Mnongodi, Chiwindi, Mpanyani, Kiromba na Mikumbi.

Kwa Upande wa wanufaika wa zawadi walimu kumi na sita shule za Msingi na Sekondari waliofanya vizuri kwenye masomo yao Mwalimu Regina Jamsoni Ndezi wa wa Mbembaleo Sekondari kwenye somo la Baolojia ameishukuru Halmashauri kwa zawadi hiyo na kutoa ahadi zaidi ya kufanya vizuri mwaka wa masomo unaondelea alisema mwalimu huyo.

Mhe Kapende aliwashauri walimu hao wasilewe Sifa kwa kufanya vizuri waone kama chachu ya kuongeza juhudi zaidi za ufundishaji wa masomo yao.

 
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa