Home » » KIJIJI CHA MABETI MISUFINI KUPATA UMEME .

KIJIJI CHA MABETI MISUFINI KUPATA UMEME .



Mbunge wa Jimbo la Tandahimba ameendelea na ziara yake ya takribani siku 15 akizungumza, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ambapo Leo katika Kata ya Litehu amesema Kijiji Cha Mabeti katika kitongoji Cha Misufini kitapata huduma ya Umeme hivi punde kwa kuwa hatua za utekelezaji wa Mradi huo zimeanza.

"Ninalo deni pale  Mabeti Misufini niwaambie tu tayari tumeshaleta nguzo Nane na Jumatatu nitashiriki Mwenyewe kuwakabidhi na niwahakikishie kuwa Umeme utawaka katika kitongoji Cha Misufini" Mhe.Katani

Katika ziara hiyo Mhe.Katani ameendelea kuwasisitiza Wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la  uboreshaji wa Daftari la Mpiga kura ili kutimiza haki yao ya Kupiga kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Mwaka huu 2024.

#kaziiendeleešŸ”„

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa