Na Chedaiwe Msuya, WF, Mtwara
Katika
mji wa Mtwara, ambao unajulikana kwa shughuli za uvuvi na rasilimali za
gesi asilia, serikali iliamua kutoa mafunzo ya elimu ya fedha kwa
wananchi, wajasiriamali, na watumishi wa serikali kwa lengo la
kuwawezesha kujikomboa kiuchumi na kusimamia vyema rasilimali zao.
Mafunzo
haya yalitolewa na Wizara ya Fedha kwa ushirikiano na taasisi za
kifedha na wataalamu wa masuala ya fedha. Wananchi waliohudhuria mafunzo
hayo walikuwa pamoja na wajasiriamali wadogo wadogo, wafanyabiashara
wadogo, na watumishi wa serikali waliotoka katika idara mbalimbali za
mji.
Miongoni
mwa washiriki alikuwa Bi. Mariam Kajewa mwanamke mjasiriamali
anayejishughulisha na biashara ndogo ndogo. Kabla ya mafunzo, Mariam
alikuwa na changamoto za kusimamia mapato yake na kudhibiti matumizi
yasiyokuwa na tija. Baada ya kushiriki mafunzo, Mariam aliweza kujifunza
mbinu za kuanzisha bajeti ya biashara yake, umuhimu wa kuweka akiba, na
jinsi ya kutumia mikopo kwa njia yenye faida.
Kwa
upande wa watumishi wa Serikali Ofisa Mifugo, Bw. Michael Kigoso,
mafunzo yatamsaidia kuboresha uwezo wake wa kusimamia mshahara wake kwa
kuweka vipaumbele vya matumizi na kuchagua njia sahihi za kuweka akiba
na kuwekeza.
Kwa
pamoja, wananchi, wajasiriamali, na watumishi wa Serikali waliohudhuria
mafunzo hayo watajikomboa kiuchumi kwa kuboresha usimamizi wao wa
fedha. Walipata uelewa zaidi wa jinsi ya kutumia rasilimali zao vizuri,
kuzuia madeni yasiyokuwa na tija, na kufanya maamuzi ya kifedha
yanayowezesha maendeleo yao binafsi na ya jamii zao.
Kupitia
elimu ya fedha, wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba mkoani
Mtwara walipata njia ya kuongeza mapato yao, kuweka akiba, na kushiriki
kikamilifu katika uchumi wa mji wao.
Serikali
pia itanufaika kwa kuwa na watumishi walio na ujuzi wa kifedha ambao
watakuwa na uwezo wa kusimamia rasilimali za umma kwa ufanisi zaidi.
Akiizungumzia
mafunzo hayo, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji wa
Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, alisema kuwa
mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha yalikuwa ni
muhimu sana katika kusaidia wananchi, wajasiriamali na watumishi wa
Mtwara kujiinua kiuchumi na kufikia malengo yao ya kifedha.
0 comments:
Post a Comment