Home » » TAARIFA ZA MIRADI ZIWE WAZI” KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO NANYAMBA.

TAARIFA ZA MIRADI ZIWE WAZI” KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO NANYAMBA.


Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Mji Nanyamba Leo tarehe 17/07/2024 yatembelea na kukagua miradi ya Maendeleo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za miradi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hamis Majali alisema “Taarifa za miradi zioneshe mapato na matumizi, faida za mradi kwa wananchi, changamoto na mikakati ya kutatua changamoto hizo; Kama kuna nguvu za wananchi zithaminishwe kwenye fedha tuone gharama nzima za mradi.”

Mhe. Majali aliwaambia wasimamizi wa miradi hiyo kuwa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ndio inayokwenda kuwasilisha taarifa kwenye Baraza la Madiwani kuwa fedha zilizotengwa kwa miradi ya maendeleo zinatumika vema au la hivyo alisisitiza uwazi wa taarifa, ukamilishwaji wa miradi kwa wakati na miradi ioneshe thamani ya fedha iliyotumika.

Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni Ujenzi wa shule ya sekondari Mtimbwilimbwi itakayokuwa na kidato cha tano na sita kata ya Mtimbwilimbwi, ukamilishwaji wa zahati ya kijiji cha Milangominne katika kata ya Milangominne, na ukamilishwaji wa zahanati ya kijiji cha Kibaoni iliyopo kata ya Dinyecha. Ikumbukwe, Zahanati ya Milangominne iliwekwa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru 2024.

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa