Home » » KATA YA MTINIKO WATAMBULISHWA MRADI WA UJENZI WA KIDATO CHA TANO NA SITA.

KATA YA MTINIKO WATAMBULISHWA MRADI WA UJENZI WA KIDATO CHA TANO NA SITA.

Kaimu Mkurugenzi Ndg Walyama Sospeter na Kamati ya ufuatiliaji wa miradi Mji Nanyamba leo tarehe 24/7/2024  Imeutambalisha ujenzi wa mradi wa kitado cha tano na sita unaotarajiwa kujengwa Katika kata hiyo ya Mtiniko.

Kaimu Mkurugenzi akitambulisha mradi huo wenye thamani ya milioni 464 aliewaleza wananchi wa kata hiyo ya kuwa Serikali imeboresha shule hiyo kwa kuongeza wanafunzi wa kidato cha tano na sita kwahiyo wananchi wajitokeze kushiriki kwenye kaziza kujitolea ili mwaka 2025 wanafunzi waanze kutumia miundombinu hiyo.

Nae mratibu wa mradi huo Mwalimu Sadiki Mashina aliwaeleza wananchi kuwa miundombinu inayotarajiwa kujengwa hapo ni nyumba ya Mwalimu 1 kwa 2, vyumba vya madarasa manne, Mabweni mawili pamoja na matundu ya Vyoo kumi.

Kwa niaba ya wananchi wa kata ya Mtiniko Diwani wa kata ya Mtiniko Mhe Saidi Makutubu aliwaleza wananchi kuwa mradi huo umeshatambulishwa kwao haina budi kujitoa usiku na mchana ili uweze kukamilika


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa