Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, amewataka madiwani wanawake,
kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yao ya kazi kikamilifu
ili kuweza kufikia malengo ya milenia.
Ushauri huo umetolewa hivi karibuni kwenye ufunguzi wa mafunzo ya
siku moja ya malengo ya milenia kwa madiwani wanawake wa mkoa wa Mtwara,
yaliyofanyika mkoani hapa.
Ndile alisema kuwa madiwani wana wajibu mkubwa katika kufanya kazi
kwa ufanisi wa kuwasaidia wanawake wengine na wananchi kwa ujumla bila
kuwa na upendeleo katika jamii inayowazunguka.
Alisema viongozi wanapaswa kujituma na kuwa mstari wa mbele katika
kutimiza majukumu yao kwani jamii imewapa dhamana kubwa ya kuwaongoza
kwenye mitaa yao.
“Viongozi tuna kazi kubwa sana ya kuisaidia jamii ambayo ndio
imetuchagua kwani jukumu la kwanza ni kuhakikisha matokeo chanya
yanamgusa mtu ndio maana hali inapokuwa mbaya katika jamii, lawama zote
zinaenda kwa viongozi.
“Ujuzi hauzeeki hata siku moja na elimu ni ya uzoefu utakayoipata ni
ya vitabuni lakini pia ya mikutano na makongamano kama haya tulikuwa
hatujui mambo ya malengo ya milenia lakini leo tutayajua, kwa hiyo
tunaweza kuwa na sauti katika bajeti katika vikao,”alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment