Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MZEE Saidi Kupwaja, mkazi wa Chikongola mkoani hapa, amepatiwa
msaada wa vitu mbalimbali baada ya nyumba yake kuungua moto Agosti 9
mwaka huu, majira ya saa saba mchana.
Akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya
Mtwara, Wilman Ndile, alisema kuwa msaada huo umetolewa na wananchi kwa
kushirikiana na ofisi yake.
Ndile alikabidhi bati 70, mifuko 15 ya kilo 50 za mchele, mifuko 10
ya kilo 50 za unga wa sembe, mfuko mmoja wa sukari kilo 50 na mafuta ya
kula ndoo tatu.
“Niliposikia hili janga la moto kwa mzee wetu nilisikitika sana na
nilikuwa safari ya kikazi nje ya Mtwara lakini baada ya kurudi
nilikutana na kitu cha ajabu kweli.
“Tofauti na majanga ambayo yanaikuta wilaya ya Mtwara toka nimeingia
hapa kama Mkuu wa wilaya kwani wananchi mlianza kumchangia mzee wetu,”
alisema.
Kwa upande wa Mzee Kupwaja, aliwashukuru wananchi wa Mtwara kwa
msaada wao na kueleza kuwa utamsaidia kutokana na kuunguliwa na kila
kitu.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment