Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI mkoani Mtwara, imeondoa kimya kimya amri yake ya kuzuia
mikusanyiko ya kisiasa na kidini na kueleza kuwa mikutano hiyo
itaendelea kulingana na taratibu zilizopo.
Wakati Mtwara ukibainisha kuondolewa kwa zuio hilo lililowekwa
kudhibiti hali tete ya vurugu za wananchi kupinga gesi asilia
isiondolewe huko bila kueleimishwa watanufaikaje, uongozi wa mkoa wa
Lindi ameendelea kushikwa na kigugumizi juu ya amri hiyo.
Wakizungumza na gazeti hili, wakuu wa mikoa hiyo, Kanal mstaafu,
Joseph Simbakalia (Mtwara) na Ludovick Mwananzila (Lindi), kila mmoja
alikuwa na majibu tofauti nay ale ya awali walipozuia mikusanyiko hiyo.
Kanal Simbakalia alisema si sahihi watu kusema katika mkoa wa Mtwara
kuna zuio la mikutano ya hadhara kwa kuwa mikutano hiyo inafanyika na
itaendelea kufanyika kulingana na utaratibu uliopo.
Alisema katika mkoa wake, mikutano hiyo ilipigwa marufuku kutokana na
hali iliyokuwepo awali ya wananchi kuandamana na kusababisha uvunjifu
wa amani na kwamba sasa kila atakayeomba kufanya mikusanyiko ya aina
hiyo ataangaliwa ana dhamira ya namna gani.
“Kuna uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa na madiwani ulifanyia na
wanasiasa walishiriki pia shughuli zao zitaendelea kwa uwazi kulingana
na namna hali ya usalama itakavyokuwa,”alisema.
Alipoulizwa ni mazingira gani yanaweza kusababisha mikutano hiyo
kuzuiliwa, Simbakalia alisema hiyo ni siri ya vyombo vya ulinzi na
usalama na kwamba hawezi kutaja mazingira hayo.
Naye Mwananzila wa Lindi, alisema watu wanapaswa kutofautisha
mikutano ya kisiasa na shughuli za maendeleo huku akieleza kuwa maonesho
ya Nane nane yaliyofanyika huko kuwa ni shughuli za maendeleo.
Alisema wanasiasa wanachochea wananchi wadai gesi isitoke tofauti na
maonesho ya Nane nane aliyoeleza kuwa wananchi wanapata elimu.
Alipokumbushwa juu ya umuhimu wa wananchi kushirikishwa katika
kufanya siasa safi kwa ajili ya maendeleo, Mwananzila aliendelea
kushikilia msimamo wake kuwa siasa haichagii maendeleo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment