Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), imedhamiria
kupunguza umasikini katika familia kupitia mpango wa kunusuru kaya.
Hayo yalibainishwa mjini hapa juzi na Mkurugenzi wa Programu za
Jamii, Amadeus Kamagenge, alipotoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji, Ladislaus Mwamanga, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku 12
ya wawezeshaji wa miradi ya ujenzi kwenye mpango wa kunusuru kaya
masikini awamu ya tatu.
Katika mafunzo hayo yaliyowakutanisha washiriki kutoka Pemba,
Unguja, Lindi Manispaa, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi na Manispaa ya
Mtwara, Kamagenge alisema walengwa wa mpango huo ni kaya zinazoishi
katika mazingira hatarishi na kukabiliwa na uhaba wa chakula.
Alisema mpango huo unajumuisha pogramu za huwasilishaji miradi ya
ujenzi, kuimarisha uwezo wa kujikimu na kuendeleza miundombinu
inayolenga sekta ya elimu, afya na maji.
“Programu ya miradi ya ujenzi inatekelezwa mahususi kwa ajili ya
kunusuru walengwa kwa kuwaongeza kipato cha kaya, kila mwaka kuna fursa
za kuongeza kipato kupitia programu hii,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment