Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMPUNI
ya Nestle, tawi la Tanzania imetoa msaada wa sh milioni 10 kwa ajili ya
mradi wa kisima kirefu katika Chuo Kikuu cha Stella Maris (STEMMUCO)
cha mkoani Mtwara.
Akizungumza katika sherehe za kuanza kuchimba kisima hicho mwishoni
mwa wiki, Meneja wa Mambo ya Kisayansi na Udhibiti wa kampuni hiyo,
Masha Macatta, alisema kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali
pamoja na wadau wengine katika kushughulikia tatizo la maji.
“Kampuni inaamini ili biashara istawi kwa muda mrefu jamii
inazozihudumia ni lazima zifanikiwe na kampuni yetu tunazingatia maeneo
matatu ambayo ni lishe bora, maji na maendeleo ya vijiji,” alisema.
Kampuni hiyo kwa hapa nchini inasambaza bidhaa za maziwa ya Nido,
Nescafe, Milo na Maggi.
Mkuu wa Kitengo cha Falsafa na Maadili ya Chuo Kikuu cha Stella
Maris, Mchungaji Dk. Aidan Msafiri, aliishukuru kampuni hiyo kwa kitendo
cha kizalendo na kuonyesha dhamira ya pekee na kujitolea kwa dhati kwa
ajili ya chuo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment