Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI mkoani Mtwara wametakiwa kuchukua tahadhari wanapomuona
mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa homa ya dengue kwa kumuwahisha
hospitali ili afanyiwe vipimo mapema kwani dalili zake kama zinafanana
na ugonjwa wa malaria.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Dk. Shaibu Maarifa, alisema
katika hospitali yake hadi sasa hawajapata mgonjwa yeyote mwenye homa
ya dengue.
Alisema wanachofanya sasa ni kutoa elimu kwa madaktari na wauguzi na
watu wengine, ili wanapobaini mtu mwenye dalili za ugonjwa huo ni
vizuri akapelekwa hospitali mapema.
"Hadi sasa katika Mkoa wa Mtwara sijapokea mgonjwa yeyote wa homa ya
dengue, ila ninachowaomba wananchi wakimuona mtu yeyote mwenye dalili
za ugonjwa huo wamuwaishe hospitali haraka," alisema Dk. Maarifa.
Dalili za ugonjwa wa homa ya dengue ni homa kali, kuumwa kichwa,
hususani sehemu za macho, maumivu makali ya viungo na misuli ya mwili,
kupungukiwa maji au damu, kichefuchefu au kutapika, kutokwa na damu
kwenye fizi na sehemu za uwazi za mwili na uchovu. Ugonjwa huo huo
unaenezwa na mbu wa aina ya aedes.
Chanzo; Mwananchi
0 comments:
Post a Comment