Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaanza ziara ya siku 26
katika Mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara kukagua uhai wa chama
na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu.
Hata hivyo, duru za kisiasa zinaonyesha kuwa ziara
hiyo ni sehemu ya kuushambulia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
ambao walitoka bungeni wakati wakijadili mchakato wa Katiba Mpya wakidai
kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo. Ukawa pamoja na CCM
walikwishafanya hivyo Zanzibar.
Wakati Kinana akifanya ziara katika mikoa hiyo,
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM, Abdallah Bulembo amekwishaanza
kushambulia Mikoa ya Kusini, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na
Uenezi, Nape Nauye alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman
Kinana ataanza ziara yake Mkoa wa Tabora, ambako atatembelea wilaya zote
kuanzia Mei 8 hadi 18. Mkutano wa kwanza utaanza leo katika Wilaya ya
Igunga.
Baadaye ataendelea Mkoa wa Singida kuanzia Mei 19
hadi 26 na kumalizia Mkoa wa Manyara, ambako ataanza Mei 26 hadi Juni 3
mwaka huu.
Nape alisema pia kuwa wamemkabidhi Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda ripoti ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika Mikoa ya
Kigoma, Rukwa na Katavi ili afahamu changamoto za mikoa hiyo.
Nape alisema kuwa ripoti hiyo inahusu changamoto
na mafanikio ambayo yamebainika katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,
Kinana aliyoifanya hivi karibuni katika mikoa hiyo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment