Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Alhaji
Mohamed Sinani, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha na kuuenzi
Muungano kwa masilahi ya taifa ikiwa ni njia pekee ya kuwaenzi waasisi
wa taifa hili.
Sinani alitoa wito huo mwishoni mwa wiki wilayani Tandahimba, wakati
akipokea mbio maalumu za pikipiki kutoka kwa Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara na mbio hizo kwa Kanda ya Kusini.
“Ni vizuri tukawaenzi kwa vitendo hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Abeid Aman Karume kwa kuendelea kudumisha na kuuenzi
Muungano. Maendeleo na amani yataendelea kudumu ikiwa Muungano
utaendelea kuwepo,” alisema Sinani.
Pamoja na mambo mengine, mwenyekiti huyo aliwashukuru viongozi wa CCM wa Wilaya ya Tandahimba kwa mshikamano wao.
“Sasa nathubutu kusema CCM imekuwa imara zaidi kuliko wakati wowote
ule, chama hiki Wilaya ya Tandahimba kiko imara, kinashirikiana
vizuri, viongozi wote wako pamoja ndiyo maana kuna maendeleo, kukiwa
kuna mtafaluku kati ya viongozi maendeleo hayawezi kupatikana,”
alisema.
Mbio hizo maalumu za pikipiki zitazunguka nchi mzima, lengo likiwa kuhamasisha uzalendo miongoni mwa vijana.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment