Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MADEREVA pikipiki ‘bodaboda’ mkoani Mtwara ambao juzi waligoma
kubeba abiria kupinga kitendo cha askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza
Ghasia (FFU) kuwakamata na kuwapiga bila sababu za msingi, jana
wamerejea kutoa huduma hiyo.
Madereva hao wa bodaboda wamerejea baada ya Mkuu wa Wilata ya
Mtwara, Wilman Ndile, kuwaomba waendelee kutoa huduma hiyo na yeyote
aliyefanyiwa kitendo hicho aende ofisini kwake kuripoti.
Awali, akizungumza katika kituo cha redio cha Pride FM cha mjini
hapa, Ndile aliwaomba madereva hao kuendelea kutoa huduma kwa wananchi
na kwamba kama kuna dereva ameshambuliwa au amepigwa na askari polisi
aende katika ofisi yake au kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara
kuripoti.
“Kama kweli kuna madereva wa bodaboda ambao wanalalamika kuwa
wanashambuliwa au kupigwa na askari polisi naomba mtu atakayefanyiwa
unyama huo afike ofisini kwangu ama kwa Kamanda wa Polisi Mkoa
kuripoti.
“Baada ya kupata taarifa hiyo na kufanya uchunguzi na kujua taarifa
hiyo ni ya kweli tutamchukulia hatua kali za kisheria,” alisema Ndile.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment