Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya miundombinu ya maji ya Mamlaka (MANAWASA).
MKUU WA WILAYA YA MASASI Hajat FARIDA MGOMI alipokuwa akipanda mti wa kumbukumbu kuzindua mradi wa maji (MANAWASA) MJINI Masasi.
Na Alvan Limwagu
Mamlaka
ya maji safi na usafi wa mazingira masasi-Nachingwea (MANAWASA) inatoa
masikitiko yake kwa wakazi wa masasi kutokana na matukio yasiyo ya
kiustaharabu yanayoendelea hivi sasa ya wizi wa "MITA ZA MAJI"
zilizofungwa na wateja kwenye maeneo wanayoishi ambapo mpaka sasa tayari
mita 7 zimeshaibiwa na watu wasiojulikana kwenye mitaa ya MKUTI, JIDA
pamoja na REST CAMP hivyo Mamlaka ya MANAWASA inawaomba wakazi wote wa
mji wa
masasi wenye nia njema na huduma hii muhimu kwa wananchi kutoa
ushirikiano katika kuwafichua wezi hawa na hatimaye wafikishwe
mahakamani kwa hatua nyingine za kisheria. "EWE MKAZI WA MASASI KUMBUKA
KWAMBA HAPO AWALI MASASI HAIKUWA HIVI ILIVYO SASA KWENYE SUALA LA MAJI"
Hivyo ni vyema kila mmoja akawa mlinzi wa mwenzake ili kuifanya
miundombinu ya MANAWASA iendelee kudumu wakati wote... pia MANAWASA
inatoa wito kwa wale wenye tabia ya kuchimba mchanga karibu na mabomba
ya maji kwenye barabara kuu itokayo mtwara kuingia masasi waache mara
moja kwani kwa kufanya hivyo husababisha mabomba hayo kupasuka na maji
kushindwa kufika Masasi.
Mtwara yetu Blog
0 comments:
Post a Comment