BARAZA
la Madiwani la Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara wamepitisha
rasmi bajeti ya sh.bilioni 19.8 ambayo itatumiwa katika halmashauri
mbalimbali za maendeleo kwenye halmashauri hiyo.
Bajeti hiyo ni kwa
ajili ya mwaka wa fedha wa 2014/2015 ambayo itashughulikia miradi ya
Elimu, Miundombinu, Maji, Kilimo, Afya, Barabara na Mazingira.
Akisoma
bajeti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Masasi, Bw. Bravo
Lyapembile alisema makisio ya mapato na matumizi ya mwaka 2014/2015 kwa
Halmashauri ya Mji Masasi yameandaliwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo
mwongozo wa mpango ya bajeti ya mwaka 2014/2015, ilani ya uchaguzi ya
chama tawala ya mwaka 2010/2015 dira ya Taifa ya 2025 na malengo ya
milenia.
Bw. Bravo Lyapembile aliongeza kuwa kwa maelezo haya naomba
kuwakilisha mapendekezo ya makisio ya mapato na matumizi ya Halmashauri
ya mji wa Masasi kwa mwaka 2014/2015 kuwa sh. 19,800,977,612.00 kati ya
hizo sh. 1,738,449,000 kutoka vyanzo vyake vya mapato vya ndani pia
halmashauri yangu ya mji Masasi imekisia kutumia sh. 4,398,278,832.00
kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo ruzuku ya serikali na fedha za
Halmashauri (Own - Source).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmashauri, Bw. Andrew Mtumisha alisema nachukua, nafasi hii
kukupongeza wewe Mkurugenzi na timu yako yote kutuandalia bajeti nzuri
yenye uhalisia wa mazingira yetu bajeti ya uwazi zaidi iliyolenga
maendeleo ya wananchi wetu ambayo imegusa kila eneo
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment