“Mkapa alikuwa kiongozi makini enzi za utawala wake, alipenda mno maendeleo kwa taifa.
“Nampenda mtu yeyote mwenye nia nzuri ya kuhudumia jamii na anayeuchukia umaskini na nimehamasika zaidi kuja hapa.
“Hili ndilo eneo analotoka Rais mstaafu Mkapa, alikuwa kiongozi makini na shujaa lazima tumuunge mkono,” alieleza lowassa.
Ujenzi huo una lengo la kuendeleza shughuli za maendeleo ya wanawake na watoto mkoani Mtwara.
Lowassa alisema mwanamke akiwezeshwa anaweza kwa sababu ni mtu makini katika utendaji na hata katika upigaji kura.
Alisema yeye siku zote amekuwa akipiga vita umasikini na kuanzia sasa yuko tayari kumsaidia mtu atakayeonyesha yuko tayari.
Akisoma risala katika harambee hiyo, Joyce Haji alisema Umaki imeweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake 1,200.
Haji alisema mafunzo hayo yamewawezesha kuwa na uelewa wa namna ya kuanzisha na kuendesha biashara na miradi ya utengenezaji wa batiki,sabuni, mafuta ya kupaka, mishumaa na usindikaji wa vyakula.
Alisema mafunzo hayo yamewezesha wanachama 556 kuinua kipato cha familia.
Wengi wao wanajishughulisha na biashara ndogondogo sambamba na uazishaji wa vikundi 30 vya kuweka na kukopa ndani ya dayosisi.
Hadi sasa vikundi hivyo vimewekeza Sh 43.6 na kutoa mikopo ya Sh milioni 38.9 kwa wanachama mbalimbali bila kutegemea msaada kutoka shirika lolote au taasisi.
Chanzo;Mtanzania
0 comments:
Post a Comment