Home » » ‘Wanahabari elimisheni jamii kuhusu NHIF’

‘Wanahabari elimisheni jamii kuhusu NHIF’

na Fatuma Mnyeto, Mtwara
WAANDISHI wa habari mkoani Mtwara, wametakiwa kutumia kalamu zao kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa NHIF Mkoa wa Mtwara, Joyce Sumbwe, kwenye mafunzo ya siku moja yaliyowakutanisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali mkoani hapa.

“Hakuna watu wanaokubalika na jamii inayotuzunguka kama wanahabari, kwa mfano utasikia watu wanabishana ukiwauliza mmesikia wapi hizo taarifa?

“Wanajibu wameandika kwenye magazeti au kwenye redio kwa hiyo kupitia mafunzo haya naombeni mukawaelimishe jamii waone umuhimu wa kujiunga na mifuko hii,” alisema.

“Lengo la kuanzisha kwa mifuko hii ya NHIF na CHF ni kusaidia jamii inapougua iweze kutibiwa kiurahisi na hizi huduma huchangiwa gharama za matibabu kabla ya kuugua na uchangiaji wake wanaonufaika ni mchangiaji, mwenza wake na watoto wanne,” alisema.

Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa