Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara imemfutia shtaka la kesi ya uchochezi
iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM)Hasnein Murji .
Hatua hiyo
imekuja baada ya Wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiomba
mahakama kuifuta kesi hiyo iliposomwa Julai 3, mwaka huu kwa madai ya
kuwa hati ya mashtaka ni dhaifu kisheria na haionyeshi ni makosa yapi
mtuhumiwa aliyotenda.
Wakili
Kibatala alieleza mahakama kuwa kifungu cha 129 na 132 cha sheria ya
mwenendo wa makosa jinai ni lazima mshtakiwa aelezwe mashtaka yake wazi
wazi yanayomkabili.
Murji
alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akikabiliwa na kesi ya
uchochezi anayodaiwa kuifanya Januari 19,mwaka huu katika eneo la Ligula
mkoani hapa.
Hakimu Mkazi
Mfawidhi Dynes Lyimo alifuta shtaka hilo na kumwachia mshtakiwa huru
baada ya kesi hiyo kuahirishwa tangu Julai 3,mwaka huu.
Wakati huo huo viongozi wa upinzani Katani Ahmed Katani (33) na Saidi
Kulaga (45) wa CUF wanaokabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama,
kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Jamhuri
wamefikishwa mahakamani.
JUMA MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment