Home » » Mahakama yamwachia huru Mbunge wa CCM

Mahakama yamwachia huru Mbunge wa CCM

Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Mtwara imemwachia huru mbunge wa jimbo la Mtwara mjini kwa tikeni ya CCM 
mheshimiwa Hasinen Murji aliyekuwa anakabiliwa na shitaka la uchochezi.

Wakili wa mheshimiwa Murji bw Peter Kibatala amewaambia waandishi wa habari mjini Mtwara kuwa mahakama 
imetolea uamuzi hoja za msingi  za kisheria baada ya kubaini kuwa hati ya mashtaka ilikuwa na mapunufu.

Amesema kuwa mheshimia Murji alikuwa ameshitakiwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo 
Mheshiwa Dyness Lyimo chini ya sheria ya kanuni ya adhabu kifungu na. 390.

 Kwa upande wake mheshimiwa Murji licha ya kuishukuru mahakama kwa kutenda haki amewashukuru 
wananchi kwa mshikamano waliokuwa nao kipindi chote alichokuwa  anakabiliwa na kesi. 

Msheshiwa Murji alifikishwa mahakamani mwanzoni mwa mwezi May mwaka huu akikabiliwa na 
tuhuma za uchochezi chini ya sheria ya kanununi za adhabu kifungu na. 390.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa