Tanzania imeweza kupiga hatua katika uzalishaji wa zao la korosho
kutokana na Elimu iliyotolewa kwa wakulima na wataalamu wa utafiti wa kilimo
cha Korosho na Magonjwa ya Korosho kutoka chuo Naliendele kilichopo
mkoani Mtwara.
Dr. Louis Kasuga ameyasema hayo katika semina ya ufufuaji wa mikorosho iliyotelekezwa,
semina inayo jumuisha mikoa 3 ya mbeya,Njombe , na Ruvuma kwa kueleza mafanikio
yaliyo patikana baada ya utafiti.
Dr Louis Kasuga amesema uzalishaji wa korosho kwa Tanzania nzima
mwaka 1974-1975 ulikuwa tani 145,000lakini kutokana na magonjwa mbalimbali na
kuhama bila mpango kiasi kilishuka hadi kufikia tani 16,000 kwa mwaka kwa
katika Tanzania Nzima
Dr louis Kasuga
mtaalamu wa utafiti wa magonjwa ya korosho amesema baada ya juhudi za serekari
kufanya utafiti na kubaini chanzo cha matatizo iliweza kuongeza
uzalishaji wa korosho kutoka tani 16,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 158,000
kwa mwaka
Wakulima wa Zao la
korosho kutoka mikoa ya Njombe ,Mbeya na Ruvuma wamesema kinachosababisha
kuzorota kwa zao la korosho ni kuchelewa kwa pembejeo na ukosefu wa masoko na
bei ya uhakika.
Mgeni Rasmi katika semina hiyo Kasimu Andrew Maswaga
amesema wakulima wajue kuwa kilimo ni ajira kama walivyo ajiliwa watu wengine
Serikarini kuna kupanda na kushuka.
Katika Tanzania kuna Miti ya mikorosho ipatayo
40,000,000 na katika miti hiyo ipo mingine ambayo imeshambuliwa na magonjwa ,
asilimia 80% ya miti ya mikorosho ili pandwa mwaka 1950 jambo
linalosababisha kupungua kwa uzalishaji, kampeni zimeanza za kupanda miche
mipya ya ya kisasa pamoja na pandikizi matawi ya kisasa.
0 comments:
Post a Comment