Home » » Mbunge Murji apata dhamana

Mbunge Murji apata dhamana

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mtwara, hatimaye imetoa dhamana kwa Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji (CCM). Akisoma dhamana hiyo, Hakimu wa mahakama hiyo, Dynes Lyimo, alisema mtuhumiwa huyo atatakiwa kufika mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu. Alisema mtuhumiwa alitakiwa kudhaminiwa Juni 10, mwaka huu, lakini alishindwa kutimiza masharti.

Alisema mshitakiwa akiwa nje kwa dhamana, hatakiwi kufanya mkutano wowote bila kibali cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara. 

Alisema mali zilizowekwa dhamana, zitatunzwa na mahakama kwa mujibu wa sheria. 

Mbunge huyo, alifikishwa mahakamani saa 2:10 asubuhi, akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Katika hatua nyingine, kesi inayowakabili viongozi wa vyama vinne vya siasa, inatarajiwa kutajwa leo.

Awali viongozi hao, walikosa dhamana baada ya wakili wao kuwa safarini.

Viongozi hao ni Hassan Uledi (NCCR), Hamza Licheta (TLP), Said Kulaga CUF na Katani Ahmed Katani (CUF). 

Kwa pamoja viongozi wote, wanakabiliwa na kesi ya uchochezi, kula njama na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Mtwara na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



chanzo - mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa