seleman akiwa juu ya mizani huku kocha wake uweso akishuhudia kwa mbali nyuma
Amot juu ya mzani ikishuhudiwa na kocha wake onyango,dr madono na kocha wa matumla mzazi na ibrahim kamwe
Bakari dunda akivishwa mkanda na mbunge wa mtwara baada ya kuchukuwa ubingwa huo katika ukumbi wa makonde.
Ibrahim kamwe 'bigright' akiwa katika meza yake ya kazi na kwa nyuma na mbunge wa mtwara mh sinani akiwa na mkanda wa ubingwa
Matumla akizungumzia jambo na uongozi mzima wa TPBO kabla ya pambano lake na mkenya.
bigright akiwa na maofisa wake baada ya zoezi zima la upimaji
Kwa picha zaidi bofya read more
hamis mtupeni juu ya mizani
haruna mnyalukolo juu ya mizani
ibrahim kamwe'bigright' akimuuliza jambo issa matumla mtoto wa Rashid matumla wakati wa upimaj
ames onyango ambaye ni medalist na bingwa wa kenya akiwa na Ibrahim 'bigright'.
kocha wa black mambas ya mtwara akifuatilia moja ya pambano kwa mbali wageni toka nchi mbalimbali walikuwepo
Tamasha la kuhamasisha masumbwi mkoani mtwara lilimalizika kwa mafanikio mazuri kwa watu kuitikia na kukubali mapambano mengine mengi ya ngumi kufanyika mkoani humo.
katika tamasha hilo lililosindikizwa na pambano la ubingwa wa taifa la uzito wa unyoya kati ya Bakari mohamed'dunda wa blackmamba ya mtwara alimshinda abdala seleman wa dar es salaam,
Nae mkongwe Rashid 'snake man" matumla alimshinda kiaina yake bondia Patrick amote wa kenya katika pambano ambalo liliwasimua sana mashabiki na kuwafanya kushindwa kukaa vitini muda wote wa pambano na hasa pale mkenya alipokwenda chini kwa konde zito lililotupwa na matumla baada ya kukwepa ngumi na kutupa hilo konde kwa kushtukiza,mwanzo alianza taratibu na kuonekana kama mchovu kutokana na kitambi alichonacho na kujikwaakwaa ulingoni lakini kadiri muda ulivyosogea ndivyo alivyobadirika na kuonekana mzuri zaidi.
pambano jingine lililowaacha hoi wapenzi wa mtwara na kukaa kimyaaa na kuduwaa kwa mshangao ni la haruna mnyalukolo wa dar na ashraf wa blacmamba kwani ngumi zilipoanza tu walianza kwa nguvu sana na kutupiana makonde mfululizo yaliyomuingia kila mmoja na kupelekana chini kwa zamu na wote walivimba nyuso na kutokwa na damu baada ya kupasukapasuka mpaka mwishowe ashraf spidi na uvumilivu ulipomshinda na kukubali kuliachia pambano kwa kukataa kurudi ulingoni raundi ya nne pambano lilikuwa la raundi sita.
0 comments:
Post a Comment