Home » » Tigo yapanua huduma ya 4G LTE hadi Lindi na Mtwara

Tigo yapanua huduma ya 4G LTE hadi Lindi na Mtwara

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Habari mdau tafadhali pokea codes,

 Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles

Mtwara, Oktoba 11, 2016-
Wateja wa Tigo katika mikoa ya Lindi na Mtwara hivi sasa wanaweza kufurahia kuunganishwa na  intaneti ya kasi kufuatia  kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE  katika miji hiyo ya kusini mwa Tanzania. Teknolojia ya 4G LTE ni ya kasi takribani mara tano zaidi ya  teknolojia  ya 3G  iliyopo katika soko kwa hivi sasa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles upanuzi huo unafuatia  kuzinduliwa kwa mafanikio  kwa huduma hiyo katika miji mingine 14 nchini.
Charles anasema “Kupatikana kwa teknoplojia ya 4G  katika mikoa ya Lindi na Mtwara  kunaonesha kuwa Tigo kwa mara nyingine jinsi ilivyojikita katika kuboresha mabadiliko katika  mtindo wa maisha ya kidijitali na kuongoza kwake katika  kutoa  teknolojia ya kisasa  na ubunifu ndani ya soko.”
Huduma ya 4G LTE  inamaanisha   kurambaza kwa kasi kubwa, kupakua vitu  kutoka katika intaneti na kufanya miito ya mawasiliano ya simu kwa kuonana (skype). Hali kadhalika inawezesha wateja  kwa kiwango kikubwa  kutiririsha video na hata mikutano ya video. Hali kadhalika na matumizi mengi kama vile kufanya mkutano kwa video, ubora wa hali ya juu, blogu za video michezo na kupakua video kutoka kwenye mitandao ya jamii.
Mtwara na Lindi  ni vituo muhimu vya biashara  katika mikoa ya kusini mwa Tanzania. “Tunataraji kwamba wakazi wa Lindi na Mtwara, wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara ya korosho, uvuvi na wadau  katika sekta ya mafuta na gesi  watafurahia uzoefu wa  teknolojia ya 4G LTE na kufanya shughuli za kijamii  kwa njia ya mtandao kwa urahisi zaidi,”anafahamisha.
Anaongeza kusema, “Ninapenda kuwajulisha wateja wetu kwamba bei bei kwa ajili ya vifuurushi  vya  intaneti ya 4G LTE ni sawa na ile  ya vifurushi vya 3G, na hali kadhalika wateja wote walio na  kadi ya simu ya 4G LTE watanufaika kwa kupata GB 10 bure  watakapojiunga kwa mara ya kwanza na mtandao wa 4G LTE. Hii inamaanisha kwamba mteja mwenye thamani  anahitaji kuwa na  kifaa kinachowezessha teknolojia ya 4G LTE, ama kiwa  simu ya kisasa au kisambazio pamoja kadi ya simu. Wanaweza kubadilisha  au kupata kadi ya simu ya 4G kutoka katika maduka yetu ya Lindi na Mtwara.”
Anaarifu kuwa mipango ipo njiani  kupanua  huduma hiyo hadi kufikia mikoa  mitano iliyobakia na hivyo kuwa imesambazwa nchini kote  ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa