Home » » Mh. Majaliwa atembelea kiwanda cha kuchakata gesi, Madimba-Mtwara

Mh. Majaliwa atembelea kiwanda cha kuchakata gesi, Madimba-Mtwara

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata gesi-Madimba, Ndugu Sultan Pwaga, wengine ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dr. Medard Kalemani (Kulia kwa Waziri Mkuu) na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio (kushoto kwa Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akimsikiliza kwa makini Ndugu Stanslaus Mallya (mwenye nguo nyekundu) akitoa maelezo namna ya kuendesha mitambo kutokea chumba cha uendeshaji (Control Room)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, wengine ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dr. Medard Kalemani na Mbunge wa jimbo la Madimba, Mh. Hawa Ghasia
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TPDC pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi Halima Dendego (Kushoto kwa Waziri Mkuu) . 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) mwishoni mwa juma alifanya ziara katika mitambo ya kuchakata gesi asilia iliyopo Madimba, Mtwara.

Katika ziara hiyo, Mh. Majaliwa aliweza kujionea uwekezaji wa kimataifa uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanznaia (TPDC). Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mh. Majaliwa alisema “nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, ni jambo la fahari kuona Watanzania wakiendesha mitambo hii tena kwa umakini mkubwa”.

Akiwa kiwandani hapo, Mh. Majaliwa aliweza kuzungumza na watumishi wa TPDC na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa kutumia utaalam wao na kutambua kwamba Taifa linawategemea katika utendaji wao. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alieleza juhudi za TPDC kuuelimisha umma kuhusu sekta ndogo ya gesi na mafuta ili kuwaandaa wananchi na fursa zilizopo na zinazokuja na miradi mikubwa ya gesi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa