Mkurugenzi Idara ya Uratibu
wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akioneshwa na
Kiongozi wa Matengenezo wa Kampuni ya kuzalisha umeme M&P mkoani Mtwara,
Musa Kongola, eneo lililoathiriwa na mvua karibu na kiwanda hicho kwa
kusababisha udongo kushuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari
Eneo la nchi kavu ambalo
udongo umeshuka zaidi ya mita mia kutoka usawa wa bahari, karibu na bomba la
kusafirisha gesi na kiwanda cha kuzalisha umeme cha M&P Mnazi
bay Msimbati Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Idara ya
Uratibu wa shughuli za Kuratibu Maafa, Brig. Jen, Mbazi Msuya akikagua maafa yaliyosababishwa na
mvua katika kalvati la barabara ya mbae inayounganisha vijiji vya Mbae na
Mbawala, Mtwara Mikindani, Aprili 2015.(katikati) ni Mhandisi msaidizi wa
Halmashauri hiyo, Is-haka Mpaki
Sehemu ya Barabara ya Mbae
ambayo kalvati lake limebomolewa na mvua, barabara hiyo inaunganisha vijiji vya
Mbae na Mbawala, Mtwara Mikindani.
Mkurugenzi wa Idara ya
Kuratibu shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya
akiwaonesha viongozi wa Kampuni ya Kuzalisha umeme mkoani Mtwara M&P jinsi
ya kuzuia udongo usishuke zaidi kutoka usawa wa bahari.
Muonekano wa Alama
lilipo bomba la kusafirisha gesi, Kiwanda cha kuzalisha umeme cha M&P na
sehemu ya nchi kavu ambayo udongo umeshuka zaidi ya kilomita mia kutoka usawa
wa bahari katika eneo la Msimbati Mkoani Mtwara
0 comments:
Post a Comment