Home » » NDANDA BOYS,MASASI GIRLS,CHIDYA NA NDIKWA ZAFUNGWA KUTOKANA NA UKOSEFU WA CHAKULA

NDANDA BOYS,MASASI GIRLS,CHIDYA NA NDIKWA ZAFUNGWA KUTOKANA NA UKOSEFU WA CHAKULA


Katika Mkoa wa Mtwara, taarifa zinasema shule za sekondari zilizopo wilayani Masasi tayari zimefungwa kutokana na hali hiyo.
Shule hizo zimetajwa kuwa ni Ndanda Boys, Masasi Girls, Chidya na Ndwika.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, MTANZANIA lilishuhudia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ndanda wakirudi majumbani kwao baada ya kufungwa.
Mmoja wa wanafunzi hao, Faudy Ngunguye anayesoma kidato cha tano, alisema wamerudishwa nyumbani baada ya shule kukosa chakula.
Lakini Ofisa Elimu Mkoa wa Mtwara, Karugendo Majidu, aliiambia MTANZANIA kuwa anatambua uwepo wa uhaba wa chakula katika shule hizo, lakini hana taarifa za kufungwa.
Majidu alisema alifanya kikao na wazabuni wanaohudumia shule hizo ambao mwanzoni walisema hawawezi kuendelea kutoa huduma, lakini baadaye walikubali kuendelea kutoa chakula.
“Kama kuna shule imefungwa labda ni kwa ajili ya likizo fupi ya sikukuu tu, lakini hadi sasa sina taarifa ya shule kufungwa, labda ongea na Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Masasi anaweza kutoa taarifa sahihi zaidi,” alisema.
Alipoulizwa Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Masasi, Paula Nkane, alisema shule hizo hazijafungwa bali zilikuwa kwenye likizo fupi ambayo inaisha leo.
Akizungumzia taarifa iliyotolewa na wanafunzi wa kidato cha tano katika sekondari ya Ndada, alisema walikuwa wamebaki shuleni wakati wa likizo, hivyo kutokana na kutokuwapo kwa chakula cha kutosha wamerudishwa nyumbani hadi shule zitakapofunguliwa.
“Hilo tatizo mimi silijui ila ninachojua wanafunzi wa kidato cha tano walitakiwa kuondoka shuleni wakati wa likizo kwakuwa chakula kisingeweza kuwatosha wao na kidato cha sita ambao wako karibuni kufanya mitihani,” alisema Nkane.

CHANZO GAZETI LA MTANZANIA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa