Na. Catherine Sungura,MoHSW,Mtwara
Serikali imetenga kiasi cha shilingi billioni 75 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa Kanda ya Kusini.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Steven Kebwe alipofanya ziara ya kutembelea mradi Huo.
"serikali imedhamiria kwa dhati kutoa huduma za afya kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa,hivyo hatunabudi kuimarisha vituko vyetu vya afya"
Dkt.Kebwe alisema kwa mkoa wa mtwara wameanza ujenzi wa jengo la mapokezi na wagonjwa wa nje (OPD), pamoja na uzio wa urefu wa kilomita 2.7,jengo hilo litakua ni la ghorofa tatu na litagharimu shilingi billioni 4,ambapo hadi sasa zimetumika shilingi billioni 1.7.
"kwa mwaka huu wa fedha serikali imetenga shilingi billioni 3 na hadi kufika mwisho wa bajeti fedha zote zilizobaki zinapatikana"
Aidha,alisema kwa mwaka ujao wa fedha wizara itahakikisha imeweka fedha ya kutosha ya kukamilisha ujenzi huo.
Hatahivyo Dkt.Kebwe aliwashauri mkoa kama wadau wa hospitali hii kuwashirikisha wadau wengine to waliopo mtwara ili kuweza kuwasaidia ujenzi huo.
Alisema hivi sasa mtwara imekuwa na wageni wengi toka nje na ndani ya nchi kutokana na fursa ya gesi hivyo wahisani wengine wangependa kuchangia masuala ya afya.
Dkt.kebwa alitaja mikoa mingine iliyopiga hatua kubwa ya kujenga hospitali za rufaa ni pamoja na Singida na MaƱyara.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment