Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe.
George Mkuchika, (katikati) akiwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma
Assad (kushoto) pamoja na wajumbe wengine wakiimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa
Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika
jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni
rasmi wakati wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi
ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach
iliyoko mkoani Mtwara.
Mgeni rasmi, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika, akiwahutubia wajumbe
wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi muda mchache
kabla ya kulifungua baraza hilo jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach
iliyoko mkoani Mtwara.
Wajumbe wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika
(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa baraza hilo uliofanyika jana katika
Ukumbi wa Hoteli ya Naf Beach iliyoko mkoani Mtwara. (PICHA ZOTE NA SARAH REUBEN - OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (Mb) amefungua mkutano
wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi uliofanyika jana
mkoani Mtwara.
Katika
mkutano huo, Waziri Mkuchika ameipongeza ofisi hiyo kwa kufanya ukaguzi wenye
viwango vya juu na hatimaye kupungua kwa hati chafu au zenye mashaka katika Serikali
Kuu na Serikali za Mitaa.
"Mimi
binafsi najivunia sana kutokana na
jitihada na mafanikio ya kazi za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayo yameijengea
heshima nchi yetu na ulimwengu kwa ujumla, licha ya kupungua kwa hati chafu, hivi
sasa Nchi yetu, ikiwakilishwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, inakagua shughuli
za Umoja wa Mataifa jambo ambalo ni la kujivunia sana", amesema Waziri
Mkuchika.
Mkuchika
ameongeza kuwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni chombo nyeti sana, si hapa Tanzania
tu bali katika nchi zote zinazozingatia demokrasia,uwajibikaji na uwazi, katika mapato na matumizi ya rasilimali za umma ili kuleta maendeleo ya
watu wake.
Akizungumza
wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma
Assad amesema mkutano huo una dhumuni la kutoa fursa kwa watumishi,
kupitia wawakilishi wao, kujadiliana juu
ya masuala mbalimbali ya msingi yanayohusu tija na ufanisi mahali pa kazi.
"
Dhana ya kuwa na Mabaraza ya Wafanyakazi
katika sehemu za kazi, hasa katika utumishi wa umma ina lengo la kutoa fursa kwa watumishi,
kupitia wawakilishi wao, kujadiliana juu
ya masuala mbalimbali ya msingi yanayohusu tija na ufanisi kwa upande mmoja na
upande mwingine maslahi yao kama watumishi", amesema Prof. Assad.
Prof.
Assad amefafanua kuwa mkutano huu wa Baraza la Wafanyakazi utatumika kujadili
malengo na mipango ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ikiwa ni pamoja na Maslahi ya
Watumishi kwa ujumla.
Mkutano
wa Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi utamalizika leo
jioni ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Weledi na nidhamu katika kutekeleza
majukumu ya Utumishi wa Umma ni chachu ya kutoa huduma bora kwa wananchi.”
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote -tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment