Serikali
wilayani mkinga imepiga marufuku wakulima kusafirisha zao la korosho
kwenda nchi jirani ya kenya bila kuwa na kibali cha bodi ya korosho
nchini tawi la tanga kwa lengo la kukwepa ushuru na badala yake watumie
utaratibu uliowekwa na serikali wa stakabadhi ghalani ambao
utawanufaisha wakulima na kuuza bidhaa hiyo kwa tija.
Akizungumza na wakulima wa zao hilo katika uzinduzi wa kuuza na
kununua korosho kwa mnada ulioanishwa na serikali na kuzinduliwa katika
kata ya duga maforoni,mkuu wa wilaya ya mkinga Bibi Mboni Mgaza
amewashauri wakulima kukataa mbinu zinazofanywa na baadhi ya
wafanyabiashara kutoka maeneo mbali mbali kwenda vijijjini kuwarubuni
ili waweze kuwauzia kwa bei isiyokuwa na tija.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wameiomba serikali kuelekeza
nguvu zake kwa kuwapelekea pembejeo za kilimo pamoja na maafisa ugani
ili kuliza zao hilo kwa tija huku baadhi ya wafanyabiashara wa zao la
korosho waliochaguliwa na serikali chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani
ambao husafirisha kupeleka katika masoko ya kimataifa katika nchi za
ASIA wakilalamikia kuwa bidhaa hiyo inapaswa kuwa na ubora kwa sababu
kuna ushindani mkubwa baina ya nchi za afrika hatua ambayo inaweza
kuharibu sifa ya zao hilo kwa nchi nzima .
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA
0 comments:
Post a Comment