Home » » WADAU WATAKIWA KUUNGANA VITA DHIDI YA VVU

WADAU WATAKIWA KUUNGANA VITA DHIDI YA VVU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MGANGA Mkuu wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Dk. Godfrey Njile, amewataka wadau nchini kuungana, ili kupambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Dk Njile alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika kwenye ukumbi wa Veta mkoani hapa, iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, kwa kushirikiana na Shirika la PSI-Tanzania, ambayo iliwakutanisha  wadau mbalimbali  kwa lengo  la  kujadili usambazaji wa bidhaa za afya kwa wananchi katika manispaa hiyo.
Alisema maambukizi ya VVU yana changamoto kubwa katika mazingira yao kwa sababu wa muingiliano wa watu umeongezeka kutokana na shughuli za kibiashara, uchumi na maendeleo kwa ujumla, ila lengo la halmashauri ni kupunguza maambukizi kwa kadri inavyowezekana.
“Lengo la halmshauri ni kupunguza maambukizi ya VVU kwa kadri inavyoowezekana, kwani madhara ya Ukimwi hayachagui yanakumba umri wowote …katika kupambana na VVU tupambane vile vile kwa kushirikiana kwa pamoja na wadau wote, kwa maana ya kwamba hakuna ambaye yuko salama,” alisema Dk. Njile.
Meneja wa la PSI-Tanzania, mikoa ya Lindi na Mtwara, Cyprian Lungu, alisema shirika lao limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ili kuwawezesha Watanzania kuwa na afya bora
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mtwara yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa