Mwenyekiti
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of
Industries), Alhaji Aliko Dangote akiwa kwenye gari huku akipata maelezo
ya ujenzi wa kiwanda hicho kutoka kwa mafundi na wahandisi ya Dil &
Sinoma inayojenga kiwanda hicho kitakachokuwa cha tatu kwa ukubwa
Afrika.
Msafara
wa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote
Groupof Industries), Alhaji Aliko Dangote, ukikagua ujenzi wa kiwanda
hicho kinachotarajiwakuanza kazi Aprili, mwakani. Awamu ya kwanza ya
kiwanda hicho ujenzi wake ukikamilikakitakuwa kinazalisha tani 6000 kwa
siku.
Dangote akiangalia moja ya majengo yanayoendelea kujengwa kiwandani hapo
Mwenyekiti
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of
Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka
Nigeria, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kiwanda kikubwa cha cha saruji
cha Dangote Tanzania, Daljit Singh (katikati), alipotembelea na kukagua
maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho,mkoani Mtwara. Kushoto ni Kenneth
Kasigila ambaye ni Msaidizi Maalumu wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB,
iliyopewa fursa ya kwanza kujenga benki karibu na kiwanda hicho.
Mkuu
wa Wilaya ya Tandahimba, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
Ponsiano Nyami (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko
Dangote, muda mfupi kabla ya mfanyabiashara huyo kuondoka Uwanja wa
Ndege wa Mtwara jana, baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda chake.
Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Dongote akiagana na Kaimu Mkuu wa Mkoawa Mtwara, Ponsiano Nyami
Mwenyekiti
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of
Industries), Alhaji Aliko Dangote, akiaga alipokuwa akiondoka na ndege
yake kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana. Alitumia takribani saa mbili
kuwepo nchini, baada ya kuwasili asubuhi saa 1:42 na kuondoka saa 3:42
baada ya kupata maelezo ya ujenzi na kukagua kiwanda chake.
Ndege ikiwa imepaa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment