Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU
wa Mkoa (RC) wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia, amekataa
kuipokea barabara ya Zambia Mikindani kutokana na kutokamilika kwa
wakati.
Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha kwanza cha Bodi
ya Barabara Mkoa wa Mtwara mwaka wa fedha 2014/2015, kilichofanyika
ukumbi wa Boma mkoani hapa.
Kanali Simbakalia, alisema amewapa siku saba warudi wakamuandalie
maelezo upya wakieleza sababu ya barabara hiyo kuchelewa kukamilika kwa
muda uliyopangwa.
“Yule mkandarasi miezi mitatu kabla ya kukabidhi barabara, zaidi ya
nusu ya vifaa ambavyo vilitakiwa viwepo kwa ajili ya ujenzi havikuwepo
na maabara ya ‘ku taste material’ haikuwepo, hiyo si sababu ya msingi ya
kuchelewesha barabara, halafu wanasema miundombinu ilikuwa shida…Sasa
swali linakuja alifanya hivyo kwa sababu alikuwa hana vifaa hivyo ikiwa
na maana wakati anaomba zabuni hakusema ukweli au kafanya makusudi,
vifaa anavyo hakuleta, ni kipi kati ya hayo mawili? alihoji Simbakalia
na kuongeza:
Taarifa yenu siikubali kuhusiana na barabara hii, hayo unayoniambia
muandike kwa sababu maandishi yapo kwa nini tuandikie mate
bwana…Andikeni upya maelezo ya kwa nini kumekuwepo na ucheleweshaji
kwenye ujenzi wa hiyo barabara, barabara ni muhimu, huu mji mkuu ndio
uso wa mkoa wa Mtwara, sasa barabara ilitakiwa ikabidhiwe mwezi wa pili
mwaka jana, leo mwezi wa nane 2014, sasa mimi nataka majibu ya uhakika
na ya kweli mniletee nione halafu nitaileta taarifa hiyo kwenye kikao
kijacho.
Kwa upande wake, Mhandisi wa Manispaa ya Mtwara-Mkindani, Francis
Rugemalila, alijitetea kwamba, kuchelewesha kwa barabara ya Zambia
Mikindani, alisema kulikuwepo na matatizo ya huo mradi ikiwemo
miundombinu na mtaalamu mshauri.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment