Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BENKI ya Afrika, Tawi la Mtwara imetoa msaada wa vitabu 118 vyenye
thamani ya sh. milioni 1.4 kwa Shule ya Sekondari ya Bandari ya mkoani
hapa.
Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo, Meneja wa benki hiyo,
Godfrey Chilewa, alisema kuwa banki yao imekuwa ikisaidia vitabu kwa
shule mbalimbali za umma zenye mahitaji ikiwa ni sehemu ya kurudisha
faida walioipata kwa wananchi.
“Sisi tawi la Mtwara tuliona vema kusaidia wanafunzi wa shule yenu
hasa kwa kuzingatia kuwa ni shule mpya na mna changamoto vyingi ikiwemo
vitabu.
“Ndugu zangu mtakubaliana nami kwamba shule zetu nyingi hususani za
umma bado zina changamoto nyingi zinazotokana na uwezo wa serikali zetu
za nchi zinazoendelea kushindwa kumudu kwa asilimia 100 gharama zote za
maendeleo ikiwemo elimu,” alisema.
Chilewa alisema kuwa kwa mwaka huu wamelenga kusaidia vitabu vyenye
thamani ya sh.milioni 15 katika shule mbalimbali nchini na kwa miaka
ijayo wataangalia miundombinu mingine lengo likiwa kusaidia shule za
umma ambazo zina changamoto nyingi.
Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Somoe Ismail, aliishukuru benki hiyo
kwa msaada huo na kuomba watu wengine kujitokeza kuisaidia shule hiyo
ambayo ni mpya ikiwa na kidato cha kwanza pekee.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment