Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TIMU ya Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF ) kutoka jijini Dar es
Salaam, juzi walitandikwa mabao 5-1 na Waandishi wa habari mkoani hapa
katika mechi ya kirafiki iliyochezwa uwanjwa wa Chuo cha Ualimu, mjini
hapa.
Katika mechi hiyo, timu ya Waandishi wa Mtwara walitangulia kupata bao
dakika ya tatu likifungwa na Oscar Nachinguru kabla ya kuongeza la pili
dakika ya sita.
Mabao hayo yalizidi kuwapa ari Mtwara kwani dakika ya 17 ya kipindi
cha pili, Juma Abderahamani aliifungia bao la tatu baada ya Mohamedi
Mchokoleka kuchezewa rafu mbaya ndani ya boksi.
Dakika ya 25, Mchokoleka aliwafungia Mtwara bao la nne kabla ya
Ramadhani Mohamedi kufunga la tano katika dakika ya 30 za kipindi cha
pili huku Wahariri walikosa penati, baada ya kipa wa Mtwara, Moses
Mpunga kupangua.
Hata hivyo, dakika ya 27 timu ya Wahariri nao walipata bao la kufutia machozi likifungwa na Kulwa Karedia.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mchezo huo, Mwenyekiti wa Jukwaa
la Wahariri Nchini(TEF), Absalom Kibanda, alisema mechi ilikuwa nzuri
na kusema kuwa kikwazo cha ushindi kwao alikuwa ni kipa wa Mtwara.
Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mtwara
(MTPC), Hassani Simba, alisema waliona burudani waliyokuwa wakiisubiri
kwa muda mrefu
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment