Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Aidha, wameitaka serikali kuwa makini katika utekelezaji wa sera na
sheria ambazo baadhi yake zimeshafanyiwa marekebisho ili kuepuka na
urasimu na vitendo vya rushwa.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana na wawakilishi kutoka kampuni na
sekta mbalimbali binafsi katika mkutano wa kutoa maoni kuhusu misingi 12
iliyopo kwenye Mkataba wa Taifa wa Maliasili nchini (TNRC).
Mchakato wa kupitia misingi hiyo iliyomo kwenye mkataba huo ambao
unaeleza namna Watanzania na taifa kwa ujumla, wanavyoweza kunufaika na
rasilimali zilizopo nchini zikiwamo gesi asilia, mafuta na madini,
ulizinduliwa mwaka jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Wakitoa maoni yao katika mkutano huo uliofanyika jana jijini Dar es
Salaam, chini ya uratibu wa Taasisi ya Uongozi nchini, walisema
wawekezaji wanakimbia nchini kutokana na mazingira ya uwekezaji kutokuwa
mazuri, zikiwamo sera na sheria zake.
Pia walihoji iwapo maoni yaliyotolewa kwa ajili ya kuboresha eneo
hilo, yatafanyiwa kazi kwa madai ya kwamba tayari mikataba imetolewa kwa
wawekezaji na halmashauri.
Balyoruguru alihoji iwapo maoni yanayotolewa kutoka makundi
mbalimbali kuhusu namna wazawa watakavyoweza kunufaika na rasilimali
hizo kwa madai ya kwamba tayari wawekezaji wameshaingia mkataba na
serikali pamoja na halmashauri.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Tan Discovery-Mineral Consultancy
Company Limited, Rogers Sezinga, alisema, sekta zote za serikali zina
sera na sheria za lakini hakuna mpango wa utekelezaji na kwamba serikali
inapaswa kufanya maamuzi kwenye eneo hilo ili kuboresha mazingira ya
uwekezaji na kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali hizo.
“Idara za serikali zina mipango na sera nzuri za maendeleo lakini
hakuna utekelezaji, kuna upotevu mkubwa katika uvunaji wa rasilimali za
nchi,” alisema.
Kwa mujibu wa Sezinga, nusu ya wawekezaji wanaondoka nchini na
kwenda nchi nyingine kwa madai kuwa serikali haina uwekezaji wa kutosha
kwenye migodi na kutokana na hilo migodi mingi ya madini ipo mbioni
kufungwa kwa siku za usoni.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi nchini, Prof. Joseph
Semboja, wakati akitoa utangulizi katika mkutano huo, alisema, iwapo
hakutakuwapo na usimamizi mzuri wa rasilimali hizo, itakuwa ni majuto
kwa Watanzania bali zikisimamiwa vizuri, wananchi watakwenda kunufaika
nazo.
Kwa upande wake mtafiti kiongozi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Prof. Amon Mbelle, alizitaka sekta binafsi kutoa maoni ambayo
yatasaidia kuimarisha mfumo bora wa utoaji maamuzi na kuangalia sababu
zinazofanya kuwapo kwa mapengo zikiwamo taarifa za ukuaji wa uchumi
usioendana na hali halisi ya maisha iliyopo.
Alitaka watoa maoni hao pia kuangalia mapengo mengine yakiwamo ya kuwa na matumizi makubwa yanayozidi mapato.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment