Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NAIBU
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Cherles Tizeba, ameitaka Mamlaka ya Usimamizi
wa Bandari Tanzania (TPA), mkoani Mtwara, kusimamia kwa umakini
uimarishaji ulinzi kwenye bandari hiyo.
Agizo hilo, alilitoa hivi karibuni mkoani hapa katika ziara yake ya
siku moja wakati akizungumza na wafanyakazi wa Bandari Mtwara.
Dk. Tizeba alisema kuwa, ni vizuri wakaimarisha ulinzi katika eneo la
bandarini ili isije ikawa kama Dar es Salaam kipindi cha nyuma.
“Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa na sifa mbaya kweli miaka miwili tu
iliyopita, watu walikuwa magari yao badala ya kushushia Dar es Salaam
pale, anapeleka Mombasa, mwingine anaona bora aende Afrika Kusini kwa
sababu ana ofu likifika Dar Sa res Salaam litakuwa limechomolewa vifaa
vyote,” alisema Tizeba na kuongeza:
“Mtwara tunaelekea huko, hivi karibuni tu mtaanza kupata meli za
kushusha bidhaa za namna hiyo hapa, sasa tusirudi kwenye hadithi ya Dar
es Salaam…Dar es Salaam ilikuwa ukinunua gari Dubai unatoa vitu vyote
muhimu unabeba kwenye ndege kwa sababu ukiacha kwenye gari huvikuti ila
hayo mambo yamekwisha sasa,” alisema.
“Sasa haya mambo yasije yakahamia hapa Mtwara, Dar es Salaam
yalikwisha kwa sababu ya hatua mchanganyiko zilizochukuliwa ikiwemo
fukuza fukuza pamoja na kamata kamata na kuimarisha mfumo wa ulinzi wa
bandari yenyewe… Nimefanya uchunguzi wangu hapa Mtwara hakuna ulinzi
kama wa Dar es Salaam, sasa na nyinyi imarisheni ulinzi zaidi,” alisema.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Bandari Mtwara, Hebel Tackson, alisema
kuwa, TPA imedhamiria kuboresha bandari ya Mtwara na bandari ndogo za
Lindi na Kilwa ili kunufaika na fursa kubwa zilizopo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari, Oliva Maeda,
alisema serikali iangalie suala la ukataji wa kodi kwenye mishahara,
kwani inawakandamiza wafanyakazi.
“Mfanyakazi anakatwa kodi katika kila kipato anachokipata,
anajitahidi kwenye mshahara anakatwa kodi, akisema afanye ‘over time’
kwa kulizalishia shirika na yeye akitegemea atapata kidogo pale, lakini
bado ‘over time’ anakatwa kodi pia, sasa cha kusikitisha sana hata mafao
yake ya mwisho anakatwa kodi…Tunaomba serikali muliangalie vizuri kwa
macho matatu suala la kodi ni kilio cha muda mrefu kwa wafanyakazi,”
alisema Maeda.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment