Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKAZI wa mikoa ya Kanda ya Kusini, wamehimizwa kuchangia damu mara
kwa mara, ili kuokoa maisha ya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto
wenye umri chini ya miaka mitano.
Ushauri huo ulitolewa mjini hapa juzi na Meneja wa Damu Salama Kanda ya Kusini, Dk. Vicent Mtweve, alipozungumza na Tanzania Daima kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani ambayo yatafanyika Juni 14.
Alisema uchangiaji damu wa kila mara unasaidia kuokoa maisha ya
wagonjwa wenye uhitaji wa damu salama na kupunguza vifo vya wajawazito,
watoto na wagonjwa wengine.
Dk. Mtweve alisema karibu asilimia 90 ya wachangiaji damu ni kutoka
shule za sekondari na vyuo, hivyo wanapokuwa likizo huchangia kuwapo kwa
uhaba mkubwa wa damu.
Kutokana na hali hiyo, aliwasihi wakazi wa Kanda ya Kusini ambao ni
kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi na wilaya za Tunduru na Namtumbo,
kujitokea kwa wingi katika vituo vya damu salama, ili kuchangia damu kwa
hiari.
“Katika wiki ya maadhimisho haya kumefanyika kampeni za kuelimisha na
kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na tumeendelea na
zoezi la kujitolea damu kwa hiari katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya
Masasi, Newala na Nachingwea.
“Hii ni muhimu kwa wananchi kupenda kuchangia damu kwa hiari, wasisubiri mpaka walazwe ndugu zao ndipo wachangie,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment