Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wilman Ndile, amelipa siku 14 Shirika
lisilokuwa la Kiserikali la Kimataifa la Care International Tanzania,
kuondoka katika wilaya hiyo baada ya kubainika kuwa wanasambaza mbegu
‘feki’ za ufuta kwa wakulima.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki,
Ndile alisema Care International walifika Mtwara kwa lengo la kufanya
kazi na wanawake na wakulima vijijini, wakidai wanaongeza kipato cha
wakulima kupitia ufuta.
Ndile alisema amechukua uamuzi huo baada ya kubaini kwamba shirika
hilo linasambaza mbegu za ufuta aina ya Lindi 2003 ambazo ni feki, na
tayari amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), kuwafuatilia nyendo
zao.
“Nawapa siku 14 hatutaki kuziona ofisi zao hapa kwa sababu hawana
mchango kwa wana Mtwara… siwataki Care International katika wilaya
yangu, nimepokea malalamiko ya wakulima wa Tarafa ya Mayanga na Mpapura
wakisema kwenye mashamba yao kuna mbegu za ufuta zilizosambazwa mwaka
2013/2014 zinastawi vizuri, lakini hazitoi mavuno.
“Niliwaita wasaidizi wangu Idara ya Kilimo nikawauliza kuhusu Care,
wakasema hawakushirikishwa, tumewauliza kituo cha Utafiti wa Mazao na
Maendeleo Kanda ya Kusini, Naliendele nao hawakuambiwa… tumeliona suala
hili ni zito, wanarudisha nyuma jitihada za maendeleo ya kilimo,”
alisema.
Mratibu wa Mradi wa Care International, Ofisi ya Mtwara, Morine
Kwilasa, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikuja juu akiwataka waandishi
wa habari wampatie majina yao na vyombo wanavyofanyia kazi huku
akibainisha kwamba si msemaji wa shirika hilo.
Chanzo;Tanznia Daima
0 comments:
Post a Comment