Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANAWAKE mkoani Mtwara wametakiwa kuchangamkia fursa za ujasiriliamali kutokana na wingi wa watu na makampuni ya uwekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mwenyekiti wa
muda wa Taasisi ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TAWEI), Emma Kawawa,
alisema uzinduzi wa taasisi hiyo utafanyika Mei 29 hadi 31 mjini hapa.
“Wanawake wenzangu ni vizuri tuchangamkie fursa zinajitokeza kwa sasa
na kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili kujiongezea kipato kwa
kuwa makampuni mengi yanakuja Mtwara kuwekeza… si kila kitu kitoke Dar
es Salaam, hata sisi tunaweza kufanya,” alisema Emma ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Entango.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo wa Entango, walipoanza waliwaelimisha
wanawake ambao kwa kiwango kikubwa walifuata maelekezo na hadi sasa
wamepata wanachama 560 kutoka wilaya zote za Mtwara.
Emma alisema kuwa kinamama kufanya biashara wanaweza na inawezekana
hata kama hauna elimu kinachotakiwa ni kujipa moyo na jitihada zaidi na
wasikubali kukatishwa tamaa na watu wengine.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment